Sunday, May 25, 2008

JINSI YA KUFANYA UNAPOKATA TAMAA YA KUISHI,AU MIPANGO YAKO INAPOKWAMA KATIKA MAISHA.

Kila Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke hupita katika hali ya kukata tamaa,haswa pale mambo yake yanapomwendea kombo:-

  • Wengine huchukua uamuzi mzuri kutatua jambo linalowachanganya,na kuangalia ni kwanini limekwama?,litapataje ufumbuzi? na kuangalia wengine walipitaje katika hali kama hiyo,na kuyapima hayo aliyoyapata kabla yakuyafanyia kazi, na mara tu wanapoona yanafaa wanaanza kuchukua hatua ya kufanya sawa sawa na jinsi alivyojifunza kutoka kwa watu wengine waliofanikiwa.
  • Lakini wengine hukata tamaa kabisa, na kusema hakika hili jambo limeshindikana,na hawataki hata kutafuta njia ya kutatua jambo hilo wanalosema limeshindikana,na matokeo yake kweli linashindikana.Wakati pengine jambo hilo hilo analopitia kuna mtu mwingine anapitia,na anafanikiwa,wakati wewe kwa kukata kwako tamaa limeshindikana. (TAFAKARI SANA HILI)

Kama unabisha angalia watu wote waliofanikiwa kihalali,wanapopewa nafasi ya kuzungumzia ni jinsi gani walifanikiwa utakuta wana misemo yao ya kujifariji wanapopita kwenye magumu:- Wengine husema kwangu hakuna lisiloshindikana,wengine husema kitu kisichoongea na ambacho hakina akili kitanishindaje, na Wengine haswa waliokoka husema Pamoja na MUNGU kila kitu kinawezekana.nk

JINSI GANI YA KUONDOA MAWAZO NA KUCHANGANYIKIWA.

  • Tafuta makundi mazuri na ujiunge nayo (Makanisani,Misikitini nk)
  • Tafuta aina ya vitabu,majarida,na magazeti unayopenda kusoma.
  • Tafuta michezo unayopenda kuangalia au kucheza.
  • Tafuta aina ya miziki unayopenda kusikiliza.
  • Tazama Tv,sikiliza Radio.

Kufanya hivyo itasababisha ubongo wako kufanya kazi vizuri,na ghafla utapata wazo jinsi ya kuanza kutafuta unachopitia

Utakapokuwa umetulia na kupata wazo ambalo baada ya kulichunguza unagundua litatatua tatizo lako,tumia busara katika kila hatua unayopia.Kwani nakuhakikishia hatua uliyopo ni njia MUNGU anayotumia kukusukuma ili usiendelee kukaa katika hali uliopo,hivyo hata mbali na kutumia busara kutatua hilo tatizo usiache kumwendea MUNGU kwa adabu,sio umwombe kana kwamba unayemuomba amekufungia macho,ujue ni lazima upite katika hali ya mateso,machungu,magumu,maumivu,kudharauliwa,kutegwa na namna yeyote ile ambayo mwanadamu anayepumua hastaili kutendewa au kupitia.

  • Kama huamini ninayozungumza angalia Mitume na watumishi wa MUNGU wa zamani na wa sasa,wote waliofanikiwa kubadilisha ulimwengu,chunguza jinsi MUNGU alivyowapitisha,utashangaa na kusema mbona MUNGU kwenye neno lake anasema kuwa yeye ni MUNGU wa UPENDO,AMANI NA HUANGAZA MAPITA YETU MBONA HATA WATUMISHI WAKE ANAWAACHA WAPITE KWENYE MATESO ? .La hasha rafiki yangu MUNGU ni mwema sana kupita kiasi,ndio maana kwa wema wake anaruhusu matatizo ili akukabidhi unachostahili kumiliki na mara tu unapokabidhiwa,ukitumie kwa adabu ukijua umekipata kwa uchungu.
  • Angalia wamama wajawazito,jamani tuwaheshimu wamama.Hawa wanadamu kuanzia siku mtoto anapotungwa tumboni mpaka wanajifua hupitia matatizo magumu yasioelezeka.ndio maana hata wanapoambiwa matoto wake ni mwizi hata kama ni kweli amedhibitisha,huwa hawakubali maana wanaamini watoto wao watabadilika tu,na huwa na uvumilivu wa ajabu maana wamama hukaa na watoto wao kwa muda mwingi kupita waababa.
  • Pili angalia matajiri wote waliofanikiwa kwa halali,kwasababu ya kutaabika walipopitia,mali zao hudumu vizazi na vizazi,kwasababu hutumia mali zao kwa adabu.Labda watoto au ndugu watakaorithi wazitumie ovyo ndio mali za huyo mtu hufilisika.Lakini angalia utajiri wa mapepo,bahati nasibu,migodini,rushwa na ufisadi matumizi yake makubwa hutumika pasipo adabu,wengi wao huzitumia kwenye uzinzi,ulevi kuhonga kutoa kafara na kufanya kila namna ya uchafu na ngafla hufulisika.Ni wachache sana wasiojihurumia na kutumia ovyo pesa zao walizozipata kwa kutaabika.

VITU VINAVYOTUMIKA KUMSABABISHA MWANADAMU AKATE TAMAA.

  • Maneno ya kuvunja moyo,na ya madharau :- Mtu atakuambia eti muonekano wako,au kwasababu una kilema fulani huwezi kufanya kazi fulani au jambo fulani.Wakati huyo huyo mtu anayekuambia hivyo huna tofauti naye,yaani yeye si malaika,na yeye pia ana mapungufu ambayo si kama yako ila anayo (asikudanganye mtu wewe ni wa kipekee,na usiposikiliza hayo anayokuambia utafanya jambo hilo hilo kwa ukamilifu tofauti na wengine,hivyo wakati mwingine wapende watu wanaokudharau maana wanakulazimisha ufanye kazi kwa bidii kwa uangalifu)Mfano mzuri chunguza watu wengi walioendelea ni watu waliodharaliwa maishani mwao na kutabiriwa maneno ya ajabu.Hakikisha unawaonyesha uwezo wako,ili waweze kutubu hiyo dhambi na wasiendelee tena kuwadharau watu wengine na kuwatabiria utabiri huo.
  • Watakuonyesha kuwa wao ni wa thamani sana kuliko wewe:- Hii ni mbinu ya kukuua kisaikolojia ujione wewe si wa thamani,na huwezi kufanya chochote.
  • Watakutisha na kukugombeza isivyo kawaida:- Njia hii watatumia ili kuua ujasiri wako ili usiweze kudai haki yako.
  • Hawatapenda uelimike:- Wanajua ukielimika hawataweza tena kukudanganya.

ONYO

Nashukuru umesoma huu ujumbe,tafadha naomba uyatendee kazi na uwe na nidhamu na kila senti inayopita mikononi mwako,huo ni mtaji MUNGU alioamuru upite mikononi mwako,kutatua matatizo yalio mbele yako na kuindeleza kwa maisha ya baadaye.

Kamwe usitumie hela ili kumuonyesha mwenzako kuwa unazo au ajue kuwa umemzidi,usitumie pesa kwa vitu visivyo na umuhimu,na usipende kujilinganisha na mtu mwingine,kumbuka wewe ni wa kipekee na una namna yako unayopenda kuvaa,usije ukaona mtu mwenye fani kama yako anafanya hivi ukamuiga,nakuonya utaumia (kwa ufupi weka nidhamu kwenye matumizi yako ya fedha)